S. L. P. 71442, Dar Es Salaam, Tanzania
dctwsaccos@ticts.com / dctwsaccos@gmail.com
+255 757 927 582 / +255 677 054 685

Kusuhu Sisi

Karibu DCTW SACCOS

1. DCTW SACCOS
DCTW SACCOS ni chama cha ushirika wa akiba na mikopo kilichosajiliwa kwa mujibu wa kifungu cha 27 cha sheria ya vyama vya ushirika Namba 20 ya mwaka 2003 tarehe 02/03/2006 na kupata nambari ya usajili DSR 0869, sheria ambayo imebadilishwa na kuwa Sheria ya Vyama vya Ushirika Namba 6 ya mwaka 2013. DCTW SACCOS wanachama wake wote ni wafanyakazi, na ni waajiriwa wa kampuni ya TICTS katika bandari ya Dar es salaam. Fungamanisho la pamoja (Common Bond) la DCTW SACCOS ni kuwa Mfanyakazi/Mwajiriwa wa TICTS.

2. UDHIBITI
DCTW SACCOS inaongozwa kwa kufuata Misingi Mikuu ya Ushirika iliyowekwa na Shirikisho la Vyama vya Ushirika Ulimwenguni, lakini pia kwa kufuata Sheria ya JMT ya Vyama vya Ushirika namba 6 ya mwaka 2013 na Kanuni zake, Aidha chama kina Masharti na Sera zake. Muhimu ni kwamba chama hiki kinadhibitiwa Kidemokrasia na wanachama wake ambao wameungana kwa hiari yao na kujipangia mambo yao wenyewe kulingana na mahitaji na mazingira yao.

3. HITIMISHO
DCTW kama chama na Taasisi kina Misingi ya kuanzishwa kwake, Kina Imani yake, Malengo na Mikakati.
a.) MISINGI Msingi Mkuu ni WATU, pili ni CHAMA. Kwamba taasisi hii imeanzishwa kwa misingi ya kuhakikisha ustawi wa watu na chama unapatikana.
b.) FALSAFA Falasafa yetu ni WATU, ARDHI na MAENDELEO. Tukiamini kuwa mikopo inayotolewa ikitumiwa vizuri kuwekeza katika rasilimali zilizopo kwa mfano Ardhi, watu wetu watapata maendeleo endelevu.
c.) IMANI Imani yetu kubwa ni kwa Wanachama, Elimu, Uwekezaji, Ushirikiano pamoja na Ushirikishwaji wa Vijana.
d.) MALENGO Malengo Makuu ya muda wote ni Kukuza Mtaji wa Chama na Kuboresha Huduma.
e.) MIKAKATI Mikakati itakayotuwezesha kufikia pale tunapohitaji kufika ni kuwekeza katika Elimu, Tafiti , Teknolojia na Kujali Muda.

DCTW SACCOS
KWA KIPATO ENDELEVU

Huduma zetu

Huduma zitolewazo na chama tangu kiliposajiliwa hadi hivi sasa ni:

Mkopo wa maendeleo

Kuanzia millioni 30,000,000/= kushuka chini kwa riba ya 1.5% na mkopo huu hutolewa kwa ajili ya kukiddhi mahitaji ya mda mrefu ya mwanachama,kiwango halisi cha mkopo ni mara tatu ya akiba yake iliyopo kwenye akaunti yake,na marejesho yake hayatazidi miaka mitatu.

Mkopo wa dharula

Ni kiasi cha TZS 1,500,000/= kushuka chini kwa riba 2%. Mkopo huu hutolewa kwa mwanachama kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya dhalula/ulazima kwa mwanachama,mwanachama atajaza fomu ya maombi ikionyesha kiasi cha mkopo na mda wa marejesho,kiwango cha juu hakizidi shillingi milioni moja na mda wa marejesho hautazidi miezi minne.

Mkopo wa mradi na viwanja

Mkopo huu unategemea na ukubwa wa kiwanja au mradi unao uombea mkopo.

Mkopo wa papo kwa papo

Ni 200,000/- kwa 10%. Ni mkopo wa haraka zidi ambao unaweza kupata hata ukiwa mbali na ofisi husika kwa kujaza fomu watu walio ofisini nakumtumia fedha muombaji hata akiwa nje ya mkoa atapokea fedha alizoomba kwa mujibu wa taaratibu zetu.