S. L. P. 71442, Dar Es Salaam, Tanzania
dctwsaccos@ticts.com / dctwsaccos@gmail.com
+255 757 927 582 / +255 677 054 685

Huduma

Mkopo wa maendeleo

 1. Mwanachama atakuwa na haki ya kukopa mpaka mara TATU ya baki ya Akiba yake au kulingana na uwezo wake wa kulipa. Kiwango cha juu cha mkopo kwa wanachama ni Shilingi Milioni Thelathini ( 30,000,000/= ) kwa muda usiozidi miaka minne (4) / miezi Arobaini na nane (48)
 2. Lazima mwanachama awe ametimiza angalau muda wa kuanzia miezi sita chamani
 3. Riba ya mkopo huu ni aslimia 1.5%
 4. Urejeshaji uatafanyika kupitia makato kwenye mshahara (Payroll system)
 5. Dhamana ya mkopo huu ni Ajira, Akiba za mwanachama kupitia Ofisa meneja rasilimali watu
 6. Mkopo huu unatolewa mara moja tu kwa mwezi (Tar 8-10)
 7. Mwanachama ataruhusiwa kutop up pale tu atakapoutumikia mkopo kwa angalau nusu ya mkopo na kuendelea

Mkopo wa Elimu

 1. Mkopo huu unatolewa kuanzia Shilingi sufuri hadi milioni mbili (0-2,000,000/=)
 2. Mkopo huu ni mahususi kwa ajili ya ada
 3. Riba ya mkopo huu ni aslimia 1.5%
 4. Mwanachama lazima aambatanishe fomu yenye jina na mchanganuo wa ada ya mwanafunzi yenye maelekezo ya kulipa mfano jina la shule, nambari ya akaunti, benki n.k
 5. Riba ya mkopo huu ni asilimia 1 (1%).
 6. Mkopo huu utarejeshwa kwa kipindi kisichozidi miezi sita (6)
 7. Angalau mwanachama awe na umri wa kuanzia miezi sita chamani

Mkopo wa papo kwa papo

 1. Mkopo huu ni mahususi kwa dharura za ghafla
 2. Mkopo huu unatolewa kuanzia shilingi sufuri hadi laki mbili (0-200,000/=)
 3. Mkopo huu utatolewa kwa njia ya taslimu au kwa kurushwa kupitia simu ya kiganjani
 4. Urejeshaji wa mkopo huu ni wa Taslimu
 5. Riba ya mkopo huu ni asilimia 10% ya mkopo
 6. Mkopo huu utarejeshwa kwa kipindi kisichozidi mwezi mmoja tu
 7. Kushindwa kurejesha mkopo huu kwa wakati kutaambatana na tozo ya asilimia 10% kwa kila mwezi utakaochelewesha
 8. Kwa mwanachama atakayepitiliza kutorejesha kwa kipindi cha miezi mitatu atanyimwa haki ya msingi ya kukopeshwa tena mkopo huu (black listed)

Mkopo wa Kiwanja

 1. Mkopo huu hutolewa kwa wanachama wenye uhitaji wa viwanja
 2. Masharti na vigezo vya mkopo huu utategemea na eneo na gharama ya ununuzi wa mashamba
 3. Lazima mwanachama awe na umri wa kuanzia miezi sita chamani

Mkopo wa dharula

 1. Mkopo huu unatolewa kuanzia TZS ziro/sufuri Mpaka Milioni moja laki tano tu (0-1,500,000)
 2. Muda/kikomo cha urejeshaji kisichozidi miezi minne (4)
 3. Riba ya mkopo huu ni aslilimia 2 (2%)
 4. Malipo kwa makato kwenye mshahara
 5. Hakuna top up
 6. Lazima mwanachama awe na umri wa kuanzia miezi sita chamani
 7. Mkopo huu unatolewa ndani ya saa Arobaini na nane endapo kila kitu kitaenda sawa